Msanii wa bongo flavour Alawi Junior amesema lengo lake halikuwa kumdhalilisha msanii mwenzanke Baraka Da Prince, baada ya Alawi kupost video fupi [clip] kwenye ujurasa wake wa Instagram ikionesha nyumba na kupongeza mama mkwe wake kwa ujenzi wa nyumba hiyo ulipofikia. Ni nyumba ambayo siku chache Baraka Da Prince alitangaza kuwa ni yake pale alipotembelewa na kituo cha televisheni EATV .
Alawi amezungumza hayo leo alipohojiwa na kipindi cha E-newz kinachooneshwa na kituo cha televisheni EATV na kusema "kiukweli yani mimi mwenyewe nimeshangaa nimepigiwa simu nyingi sana na watu alafu watu wengi wamenitumia sana dm Instagram nilikuwa sifshamu chochote sababu hata kwenye akaunti yangu Instagram mimi sijam'follow Baraka, na Baraka naweza nikasema ni mdogo wangu, naweza nikasema pia ni mume mwenzangu, yeye anatoka na Naj na mimi natoka na dada yake Naj. Kwahiyo sikujua kama alipost nyumba na hata ukiangalia post ambayo ali post yeye ina kama WIKI hivi nyuma na mimi nilipost jana na kiukweli mimi nilikuwa sijui. Nili'post kwasababu mimi ndiyo niliyefanya proccess za kutafuta hiyo nyumba, kwahiyo nilipo npost siku post kwa nia mbaya. Baraka ni kama mdogo wangu na hajawahi kunikosea.
No comments:
Post a Comment