Friday, 14 October 2016

KAMPUNI YA VINYWAJI BAKHRESA YAOMBA RADHI

Siku chache zilizopita kwenye mitandao ya kijamii ilisambaa picha ikionesha moja ya vinywaji vya kampuni ya Azam Bakhresa kijulikanacho kama AZAM MANGO, kikionesha kimekosewa tarehe ya siku ya uzalishaji na tarehe ya siku ya mwisho wa kutumia kinywaji hicho (Expire date)

Kinywaji kikionesha kimezalishwa tarehe tarehe 19/10/2016 na wakati ilikuwa ni tarehe 6 ambayo hata tarehe hiyo 19 ilikuwa bado haijafika.

Picha hiyo iliwashangaza wengi na kuwatia hofu ya kuhisi wanatumia bidhaa ambazo si sahihi kwa matumizi.

No comments:

Post a Comment