Monday, 10 October 2016

STAN BAKORA AELEZA UKWELI KUHUSU VIDEO COVER YA WIMBO NISAMEHE

Msanii maarufu nchini Tanzania aliyejizolea umaarufu huo kupitia sanaa ya vichekesho, ambaye anatambulika kwa jina la Stan Bakora ameamua kuuambia umma ukweli kuhusu tuhuma alizopewa na mwanamuziki Baraka Da Prince kwa kinachonakiliwa kama ni kumkashifu baada ya kutoa video cover ya wimbo ujulikanao kama #Nisamehe .

Msanii Stan Bakora alipost picha iliyoambata na ujumbe ambao ulisomeka hivi "Tangu nianze kufanya cover za wasanii , sijawahi kufanya cover ya msanii yeyote pasipo na makubaliano kati yangu mimi na msanii mwenyewe. ndivyo hivyo ilivyokuwa hata kwenye cover ya #Nisamehe ya @barakahtheprince ... Before ya kufanya tulikubaliana kwanza, sasa nashangaa kuona anapost na kuongelea kitu ambacho kama hatujakubalia






Amefanya hivyo ni kuafuatia kwa malalamiko ya msanii huyo Baraka The Prince akimtaka Stan Bakora kutotumia tena kile alikiita yeye utani kwan kusema "Matani ni mazuri ila yakizidi yanaweza kuleta matatizo... Heshima ichukue nafasi yake tafadhali mzee @stanbakora utani huu sijaupenda iwe mwanzo na mwisho tafadhali"








Hayo yote yamejitokeza ni kutokana na hiyo picha ikimuonesha Stan Bakora kuuvaa,,  uhalisia wa kimuonekano na kimavazi,  Stan Bakora alifanya video cover ya wimbo nisamehe ulioimbwa na msanii Baraka Da Prince 

No comments:

Post a Comment