Lakini tukio ambalo halikunukuliwa kwenye camera limeibua mzozo kwenye vyombo vya habari vya nchini humo.
Shabiki mmoja mwanamke anatuhumu kuwa simu yake imevunjwa alipojaribu kupiga picha 'SELFIE' alipowasili katika uwanja wa ndege Mombasa.
Kwa mujibu wa gazeti moja nchini humo ''Daily Nation'' mwanamke huyo anasema Chris Brown alimpokonya simu kwa nyuma alipojitayarisha kupiga picha hiyo na kuirusha chini .
Taarifa hiyo inaongeza kuwa simu ya msichana huyo aina ya iPhone 6 iliyomgharimu kiasi cha dola 900, haikuvunjika lakini screen guard na kifunikio cha simu viliharibiwa.
Shabiki huyo alisema amenunua tiket kuhudhuria hilo, amehudhunishwa na ameamua kutohudhuria tamasha hilo.
Tuhuma zake zimesababisha gumzo katika mtandao wa kijamii ujulikanao kama twitter ambapo Wakenya wanajadili iwapo muimbaji huyo arudishwe Marekani.
Hisia zimegawanyika ambapo wengine wanamtetea na wengine wakitaka atimuliwe Kenya.
Clip ama kipande cha cha video kilichowekwa twitter na @KinyanBoy inaonekana kumuonesha Chris Brown akipuuza ombi la mwanamke huyo kupiga selfie na anampita bila kumgusa.
Lakini mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Brenda Chepkoech, alizuzungumza na televisheni ya NTV nchini humo, anasisitiza kuwa tukio hilo baada ya clip hiyo kuwekwa kwenye mtandao na ni muda mfupi kabla Chris Brown kuingia kwenye gari na kuondoka.
No comments:
Post a Comment